Kocha Newcastle asema alunta kontinua

Muktasari:

Rafael Benitez amesema mapambano yanaendelea na kamwe hatakata tamaa katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Kocha huyo alisema atapambana kuhakikisha anamaliza ndani ya sita bora.


London, England. Licha ya kutokuwa na mwenendo mzuri katika Ligi Kuu England, Kocha wa Newcastle United, Rafael Benitez amesema wanaweza kumaliza msimu ndani ya  sita bora.

Benitez  ambaye pia amewahi kuzinoa Chelsea na Liverpool,  amekuwa katika mvutano wa muda mrefu na mmiliki wa Newcastle, Mike Ashley kwa kutotoa sapoti ya kutosha ya fedha  kinapofika kipindi cha usajili.

“Tunaweza kumaliza kwenye nafasi sita za juu katika msimamo wa ligi, kumaliza nafasi nane za juu ni kitu chepesi kwangu. Nasema rahisi kwa jambo moja au mawili.

“Nilipoamua kuja hapa, ilikuwa ni kwasababu ya shauku ya mafanikio ya klabu, mvuto wa mji na kila kitu.Bado naona ni vile vile,” alisema kocha huyo.

Benitez alisema ni ngumu kushindana na Man City na vigogo wengine kumaliza katika nafasi nne za juu kwa kuwa wana nguvu ndogo ya kiuchumi.

Kocha huyo alisema kuwa ni rahisi Liverpool, Chelsea, Tottenham Hotspurs na Arsenal kuisimamisha Man City katika mbio za kuwania ubingwa kwa kuwa ziko vizuri kiuchumi.

“Wanaweza kununua mchezaji yeyote mwenye kiwango cha juu, tofauti na timu za daraja la kati, ukiongelea Man City thamani ya kikosi chao ni zaidi ya Pauni500 milionu,”alisema Benitez.