Lifahamu Shindano la Tuje Pamoja

TUJE PAMOJA - The Kilimanjaro Project 2018

Kwa lugha nyepesi, neno “Tuje Pamoja” linahitaji kuchukau hatua, tunahitaji kuhamasisha Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za pamoja dhidi ya mabadiliko ya hali ya tabia nchi.

Tunaamini katika nguvu ya watu na jamii iliyohamasika katika kutengeneza mabadiliko ya muda mrefu, tunaamini katika kutoa matumaini na kuwezesha kila mtu kuchukua hatua katika kulinda maliasili zetu.

Tukijumuisha ushirikiano wa pamoja katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, ukataji wa misitu na kupoteza viumbe hai, Mkoa wa Kilimanjaro unaathirika kwa kiasi kikubwa; theluji juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro imepungua kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miaka 20, na kiwango cha mvua nacho kimepungua.

Mambo yote hayo kwa pamoja yamesababisha kuongeza hatari kwenye mfumo wa ikolojia na uhai wa wanyama pori, na kwa watu wanaotegemea mlima huo kuendesha maisha yao.

Kwa kupanda mamilioni ya miti na kuongeza ukubwa wa msitu kwenye eneo hilo, kiwango cha mvua kitaongezeka na miti hiyo kuongeza mali asili; kupunguza hewa ukaa na uchafuzi wa hewa kwa ujumla; kuongeza hewa ya oksijeni na kurejesha mzunguko thabiti wa viumbe hai na ikolojia katika eneo hilo.

Njia tunayotumia kufikia lengo hilo ni KUCHUKUA HATUA! Tunapanda maelfu ya miti katika lengo la kurejesha katika hali yake ya kawaida maeneo yaliyoathirika kwa ukataji misitu na uharibufu wa mazingira.

Upandaji wa miche ya asili Tanzania katika eneo zima la Mkoa wa Kilimanjaro, tukiwa na lengo la kupanua wigo wa upandaji miti hadi Dodoma kufikia mwaka 2019. Katika mwaka 2018 pekee, tumeshapanda zaidi ya miti 75,000, na tunatarajia katika kipindi cha miaka michache ijayo, itaongezeka hadi kufikia mamilioni ya miti.

Shiriki sasa Shindano la Tuje Pamoja, Ni Rahisi!

  • Bofya Hapa kutembelea ukurasa wa jinsi ya kushiriki
  • Nunua ama “mti mmoja” Kwa Tsh3,000 au “miti mingi” kwa Tsh10,000 kwa kulipia kupitia Mpesa LIPA NAMBA 5588080
  • Shirikisha mchango wako kwenye Twitter na Instagram ukitumia hashtag #TujePamoja na @thekiliproject.

Ni hivyo tu!

Unapotoa mchango wako kwenye shindano hili la Tuje Pamoja, utakuwa umeingia moja kwa moja kwenye mchuano wa kushinda safari iliyolipiwa kila kitu mwisho wa wiki na Unzip Tanzania (Kwa wale walio Single), au kwenda Ngare Sero Mountain Lodge Arusha au Melia Zanzibar; zawadi mbili maalum zitakazotolewa na wadhamini wetu!

Tusaidiane kupanda miti kuzunguka Mlima Kilimanjaro na kuufanya uwe chanzo cha mvua tena!