Mbunge Katani asema hafikirii kuondoka leo wala kesho

Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Ahmed Katani (CUF)

Muktasari:

  • Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Ahmed Katani (CUF leo Alhamisi ndani ya ukumbi wa Bunge amekanusha taarifa za yeye kujizulu bungeni

Dodoma. Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Ahmed Katani (CUF) amekanusha madai ya kujiuzulu ubunge na ameomba vyombo vilivyomnukuu kumuomba radhi haraka.

"Sifikirii kujiuzulu leo, wala kesho na hata siku yoyote labda wanaotumika waje wanifukuze wenyewe," amesema Katani

Katani ametoa kauli hiyo bungeni leo jioni Alhamisi Novemba 15, 2018 baada ya taarifa kusambaa kwamba amejizulu.

Amesema haijui hiyo barua inayotajwa kuandikwa na yeye na akasema kitendo hicho kimemdhalilisha.

Hotuba yake imekatizwa na Spika Job Ndugai baada ya kelele nyingi za kumshangilia kutoka kwa wabunge wa upinzani ndipo Spika akaomba makatibu wake wamsaidie kubaini sauti ya mbunge mwanamke aliyekuwa akipiga kelele zaidi.

Katani ataendelea kuchangia baadaye baada Spika Ndugai kumpata aliyepiga kelele na kutoa uamuzi.

Endelea kufuatilia Mwananchi