Msechu adai washindi BSS hulewa sifa

Muktasari:

Msanii wa Bongo fleva, Peter Msechu, amesema sababu ya washindi wa Bongo Star Search kushindwa kutoboa kimuziki ni kujaa sifa ya fedha wanazozipata wakishinda .


Msanii wa Bongo fleva, Peter Msechu, alisema moja ya sababu ya washindi wa Bongo Star Search kushindwa kutoboa kimuziki ni kujaa sifa ya fedha wanazozipata wakishinda .

Msechu aliyewahi kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo mwaka 2009, alisema fedha ndio sababu kubwa ya wasanii hao kushindwa kufanya vizuri kama wenzao ambao hawakufanikiwa hata kufika tano bora.

β€œSio kisa umeingia na kushinda na kujazwa mapesa basi unaona kila kitu unapaswa kufanyiwa na wewe hela ulizopewa kutumia kwa mambo mengine ikiwemo ya anasa.

β€œ Ifike mahali kila unayepata nafasi ya kuingia kwenye shindano hilo kuendelea na kile ulichodhamiria hata kama hukushinda,” alisema msanii huyo.

Baadhi ya wasanii waliwahi kupita katika shindano hilo paamoja na kutoshinda namba moja na sasa wanafanya vizuri kwenye muziki ni mbali na Msechu ni pamoja na Kala Jeremiah , Frida Amani na Baby Madaha.

Wengine ni Walter Chilambo, anayeimba muziki wa Injili na Haji Ramadhani, anayeimba muziki wa dansi katika bendi ya Twanga Pepeta.