Ray: Nitaoa tu ukifika wakati sahihi

Muktasari:

Mwigizaji Vicent Kigosi maarufu Ray amekuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu na mkali wa maigizo nchini, Chuchu Hans Ray,  amesema mashabiki wake wasiwe na haraka kwa sababu masuala ya ndoa hayahitaji kukurupuka.

Mwigizaji Vicent Kigosi maarufu Ray amekuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu na mkali wa maigizo nchini, Chuchu Hans.

Baada ya uhusiano huo kuleta matunda ya mtoto wa kiume waliyembatiza jina la Jaden, mashabiki wao wakabadili swali juu yao, je, wataoana lini?

Ray alipopiga stori na Mwananchi amesema mashabiki wake wasiwe na haraka kwa sababu masuala ya ndoa hayahitaji kukurupuka.

“Mimi nitaoa tu muda ukifika na nitaweka wazi kila kitu. Mashabiki wangu wakumbuke kuwa nipo kwenye uhusiano na Chuchu na niliweka wazi mapema sasa hata ndoa nitaweka wazi bila ya kuficha.”

Alijisikiaje siku ya kwanza kusikia chuchu anaujauzito wake?

“Siku ya kwanza kusikia Chuchu Hans ana ujauzito wangu nilijua ni mchezo tu maana mara nyingi alikuwa akipata ujauzito unaharibika, kwahi hata alivyokuja kuniambia ana ujauzito nikajua ni yale yale tu lakini siku zilivyozidi kwenda nikajua sasa ni kweli na nikasema Mungu ni mwema,maana nilikuwa ndio kilio cha muda mrefu na furaha ilizidi kupata mtoto wa jinsia nayotaka wa kiume japo mama yake alikuwa anataka wa kike

“Na naendelea kushukuru kuwa mtoto wangu kufanana na mimi, namanisha Chuchu alivyokuwa na ujauzito,mambo mengi yalikuwa yanaongelewa,mara oooh Ray mgonjwa wa Ukimwi, mara sina kizazi, sasa mungu amewaaumbua wambea na wanafki”

Yuko wapi?

Mashabiki wa filamu wanajiuliza mbona Ray siku hizi hatoi filamu mpya mfululizo, ni kimemtokea na hadi kushindwa kufanya hivyo? Wapo wanaojipa majibu kuwa, huenda majukumu ya kulea familia yamemzidi na ndio maana anashindwa kujigawa .

Mwananchi lilipomuuliza Ray ambaye jina lake halisi ni Vicent Kigosi amesema kimya kingi kina mshindo.

Lakini pia Ray alisema,kabla ya kutoa movie zake jikoni ipo filamu ameshirikishwa inaitwa Imetosha hivyo mashabiki zake waanzie kumuona hapo.

“Najua mashabiki zangu wamenimis kiasi gani,niwaambie tu nilikuwa nawaandalia kitu kizuri kwao,ila kwa sasa niwaambie tu nimerudi kwa kishindo kwa movie ya Imetosha ni movie ya Zambia na mimi nimeshirikishwa tu,” anasema.

Kuhusu mmomonyoko wa maadili

“Naomba nilizungumzie hili suala kwa ufupi kidogo, nipo tayari kumzungumzia Wema sababu tumembrand sisi wenyewe maana nakumbuka siku moja Lamada Hotel, marehemu Steven Kanumba alinifata na kuniuliza kama Wema anafaa kuwa mwigizaji, maana kulikuwa kunatakiwa waigizaji wapya wa kike wacheze filamu ya ‘A point of no Return’ ,basi tukaangalia storia

nikaona anaweza na Wema ndio ilikuwa filamu yake ya kwanza na ndio maana nasema ananihusu.

“Wema amekosea sana na sio mara ya kwanza kukosea, cha msingi ajijue yeye ni brand hivyo ajirekebishe Watanzania wanampenda asiwaangushe.”

“Kwanza kabisa nampongea Majizzo kwa kufuata ushauri wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda wa kutaka amuoe Lulu, pia nawapongea wote wawili na wawe makini maana kwenye ndoa kuna mambo mengi hivyo wanatakiwa .”