Sarafu mpya Kenya zajaa wanyamapori

Muktasari:

Katika mabadiliko ya Katiba, Wakenya walitaka sura za viongozi zilizokuwa kwenye fedha za nchi hiyo ziondolewe na badala yake ziwekwe picha za vivutio vya taifa.


Benki Kuu ya Kenya imetoa sarafu mpya ambazo zimetawaliwa na michoro ya wanyama. Sarafu hizo nne shilingi moja, tano, kumi na 20.

Urithi wa Kenya wa wanyama wa porini unaonekana dhahiri kwenye sarafu hizo ambazo zimetolewa upya kutokana na utashi wa katiba mpya inayotaka kuondolewa kwa sura za viongozi na kuweka vivutio vya nchi.

Wanyama walio katika sarafu hizo ni tembo, vifaru, twiga na simba ambazo zinaonekana upande mmoja kama ilivyo katika noti.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa sarafu hizo zilizopewa jina la "Kizazi Kipya cha sarafu".