VIDEO: Shinuna Nassir anayeigiza sauti ya Fidan Hatun

Muktasari:

Ni tamthilia inayohusu maisha ya Sultan Suleyman. Katika umri wa miaka 26 alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottomans akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great.

Ni tamthilia inayohusu maisha ya Sultan Suleyman. Katika umri wa miaka 26 alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottomans akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great. Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim….

Kuhusu Fidan Hatun

Katika tamthilia hii anaigiza kama kijakazi wa Hurrem na baadaye Mahidevran. Nafasi hiyo imechezwa na mwigizaji wa Uturuki, Gamze Dar anayefahamika nchini humo kwa kucheza filamu za The Pit, Magnificent na Eve Donus.

Shinuna Nassir (Fidan Hatun)

Mtangazaji anayenakilisha sauti ya waigizaji mbalimbali lakini leo anaizungumzia nafasi ya Fidan Hatun ambaye ni kijakazi wa Hurren.

Shinuna ni mfanyabiashara ndogondogo na mkazi wa Ilala ambaye hakuwahi kufikiria kama angekuja kufanya kazi kama hiyo.

Anasema alipenda zaidi kazi ya utangazaji ambayo hadi aliisomea, lakini katika harakati za kusaka maisha ndio hivyo amejikuta katika kazi hiyo ya kunakili sauti.

Anasema changamoto anazozipata ni katika kubadili sauti za wahusika kutoka ya Belhan Sultan na kwenda kwa Rakel Hatun kwani alikuwa kashazoea ya mhusika wa kwanza ambaye naye hakukaa sana alifariki na kupewa Fidan Hatun. Anakiri kwamba pamoja na changamoto hizo za kubadili sauti za watu watatu tofauti, anashukuru kadri siku zinavyozidi kwenda amekuwa akizoea.