Spika azipangua Kamati za Bunge

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Muktasari:

  • Spika wa Bunge Job Ndugai amepangua wajumbe wa Kamati za Bunge ambapo Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wajumbe wake saba wamehamishwa na kupelekwa katika kamati nyingine.

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amepangua wajumbe wa Kamati za Bunge ambapo wabunge saba waliokuwa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wamehamishwa na kupelekwa katika kamati nyingine.

Wajumbe waliohamishwa kutoka Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na kupelekwa kamati nyingine ni pamoja na Salim Hassan Turky (Ardhi, Maliasili na Utalii), Mansoor Hirani Shanif (Utawala na Serikali za Mitaa), Abdulaziz Abood (Miundombinu), Lucy Mayenga (Ardhi, Maliasili na Utalii) na Munde Tambwe (Miundombinu).

Wengine waliohamishwa toka katika kamati hiyo ya Viwanda, Biashara na Mazingira ni Ahmed Ally Salum (Hesabu za Serikali za Mitaa-LAAC), Diodourius Kamala (Bajeti).

Wajumbe wengine waliohamishwa ni Ibrahim Hassanali Mohamed Raza kutoka kamati ya Bunge ya Bajeti kwenda (Utawala na Serikali za Mitaa), Richard Ndassa kutoka Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwenda Viwanda, Biashara na Mazingira.

Wengine ni Jafari Sanya Jussa kutoka Ardhi, Maliasili na Utalii kwenda Viwanda, Biashara na Mazingira na Machano Othman Said kutoka Huduma na Maendeleo ya Jamii kwenda Viwanda, Biashara na Mazingira.