Tambua kuwa mkeo si rafiki yako

Muktasari:

  •  Mtaalamu wa ndoa na familia Carrie Krawiec anaeleza tofauti kati ya ndoa na urafiki, kubainisha kuwa wanaume wanapaswa kutambua kuwa mke si rafiki

Dar es Salaam. Kufikiria kuwa mkeo ni rafiki yako wa dhati sio sahihi na haimaanishi kuwa ndoa yako si bora au haiko mubashara kama Waswahili wasemavyo.

Bali ni kutambua tofauti ya mwanandoa na rafiki kwani licha ya kuwa baadhi ya vitu vinafanana lakini ni mahusiano mawili tofauti.

Wataalamu wa masuala ya uhusiano wanaonya kuwa kuchanganya vitu hivyo viwili kunaweza kuleta athari zaidi katika ndoa kuliko urafiki.

“Marafiki wengi hatuishi nao pamoja, hatuingiliani nao kiuchumi, kisheria, wala kimahusiano. Marafiki tunashikamana nao pale wanapokuwa wanahitaji kitu fulani,” Mtaalamu wa ndoa na familia Carrie Krawiec amesema na kuongeza, “wenza wana uhusiano wa moja kwa moja na ndugu, familia, ratiba na hata maisha.”

Inafikirisha sana kujua kwa nini ndoa inachanganywa na urafiki lakini imeelezwa vizuri kuwa ndoa ni nzuri kwa afya, ustawi wa mtu na umri mrefu kama ilivyo kwa urafiki.

Pia wanandoa wana matumaini kidogo kwa marafiki kuliko wasio wanandoa. Sio kwa sababu wanandoa wameingia katika jukumu la urafiki wa dhati, hapana ni kwakuwa kila mmoja anao wa kwake.

“Mwanandoa anakuwa na wazazi wa pande mbili, ndugu na watoto kama chanzo cha msaada. Wanandoa wana wigo mpana wa kusaidiana,” anaeleza Krawiec.

Hata hivyo hii ni tofauti na urafiki ndiyo maana ukikosea kimoja wapo unaweza ukaibua migogoro ndani ya ndoa na Krawiec anatahadharisha kuwa wanaume wanaotarajia wake zao kuwa marafiki zao ni kukuza matarajio yasiyowezekana kwa namna watakavyoshirikiana na maamuzi mengine.

Endapo mwanaume atadhamiria kuacha kazi ya ofisi na kuamua kuwa fundi Seremala kama kazi ambayo anashauku nayo, marafiki watampongeza na kuwa naye bega kwa bega lakini mke wake atakuwa na maswali mengi ya kuuliza.

“Pale tunapokosea mwenza huwa na maswali, wasiwasi na dukuduku, kutokana na kukosa msaada tunawapatia majukumu ya marafiki ambayo hayapaswi kufanywa nao,” anasema Krawiec.