Usipuuzie tendo la ndoa

Muktasari:

Ushawahi kujiuliza kuhusu umuhimu wa tendo la ndoa, inaelezwa kuwa hatua ya kuwa karibu na mpenzi wako kimwili husaidia kunogesha ukaribu wa wanandoa.

Kenya. Sikuwahi kufahamu umuhimu wa tendo la ndoa katika mahusiano nilipokuwa nje ya uhusiano. 

Lakini kwa sasa nimekuwa mbali sana na uhusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa, nimejifunza mazingira magumu.

Hatua ya kuwa karibu na mpenzi wako kimwili husaidia kunogesha ukaribu wa wanandoa.

Kukosekana kwa tendo la ndoa nchini Kenya kumekuwa  chanzo cha wanandoa wengi kuachana kisheria.

Tendo la ndoa limekuwa ni muhimu katika kuimarisha mahusiano ya wanandoa na familia kuwa pamoja.

Kwa upande wangu, tendo la ndoa limekuwa ni siri kubwa ndani ya hisia za moyo wangu.

Jambo la msingi ni kwamba, unaposhiriki jambo na mtu yeyote jaribu kufungua moyo wako ili wakutambue vyema. Una kitu cha ziada kitakachokusogeza katikati ya mjumuiko wa watu mbalimbali.

Umewafanya kuwa na amani kwa hiyo watakufanya kuwa sehemu ya maisha yao.