Vitambulisho vya Magufuli vyazua mambo mapya

Muktasari:

  • Rais Magufuli alitoa vitambulisho kwa ajili ya wajasiriamali wadogo kwa ajili ya utambulisho,ambapo aliwapa wakuu wa Mikoa wote nchini kwa ajili ya kuvigawa kwa wahusika.

Dar/mikoani. Uamuzi wa Rais John Magufuli kugawa vitambulisho 670,000 kwa wafanyabiashara wadogo, umesababisha hatua tofauti kutoka kwa wateule, wafanyabiashara na wadau.

Wako wakuu wa mikoa waliopitiliza vituoni kwao kuvigawa, wako waliopanga siku za mbeleni, huku wafanyabiashara wakieleza hatua hiyo ya Rais ingeambatana na “kulegeza vyuma”, kulainisha mzunguko wa fedha na wengine kulalamikia urasimu wa watendaji.

Wapo pia waliosema kuwa katiba inaliruhusu Bunge tu kupanga, kupunguza na kupandisha kodi.

Hayo yamebainika katika uchunguzi uliofanywa na Mwananchi baada ya Rais kuwashtukiza wakuu wa mikoa na watendaji wa Mamlaka ya Mapato (TRA) juzi kwa kuibuka ukumbini na vitambulisho hivyo alivyosema amevichapisha mwenyewe baada ya kuona kasi ndogo ya kutambua “wamachinga”.

Alisema mfanyabiashara yeyote, ambaye mapato yake kwa mwaka hayazidi Sh4 milioni, atakayekuwa na kitambulisho hicho, asibughudhiwe.

Baadhi ya wajasiriamali waliohojiwa na Mwananchi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Mbeya, walishukuru kuwa sasa wamepata utambulisho, wengine wakasema hilo pekee halitoshi na wengine kuhoji kama watendaji wanamuelewa mkuu wa nchi.

“Lengo ni zuri na vitambulisho hivi vitatusaidia kutambulika,” alisema Heri Mkumbukwa anayeuza matunda katika soko la Mabibo, Dar es Salaam.

“Mwanzoni tulikuwa tunakamatwa ovyo na kutozwa ushuru wa kila aina. Sijui vitambulisho hivi vitatusaidiaje kukuza biashara zetu kwa kuwa hali bado ngumu.

“Biashara haiendi jambo linaloweza kusababisha tukaviweka kama mapambo.”

Mfanyabiashara mwingine anayeuza nguo eneo la Buguruni, Simon Maghembe alisema vitambulisho hivyo vitasaidia kupunguza manyanyaso ya mgambo wa jiji, lakini akalalamikia gharama yake.

“Wafanyabiashara wadogo tuna matabaka. Kwa wengine Sh20,000 ni kubwa, Rais angeipunguza kidogo…walau iwe Sh10,000,” alisema.

Hatua hiyo ya Rais pia ilipokelewa kwa mtazamo huo mkoani Morogoro, ambako wafanyabiashara pia wamekuwa wakisumbuliwa na mamlaka.

“Mfano wamachinga wa Kariakoo hawasumbuliwi kwa sababu Serikali imewawekea mazingira mazuri ya kufanyia biashara,” alisema Leonard Yona, mmoja wa wafanyabiashara wa mjini Morogoro.

“Wamewatengea maeneo rafiki na yenye mkusanyiko wa watu hata suala la ushuru wako tayari kulipa lakini si kwa hapa Morogoro.” alisema Yona.

Mjini Moshi, Alhaji Abdala anayeuza urembo eneo la stendi kuu, alisema hofu yao baada ya kupata vitambulisho hivyo ni kutakiwa kulipa kodi.

“Unaweza upewe kitambulisho halafu ukaambiwa utafute mahali pa kufanyia biashara, kwa kuwa stendi pana uongozi na utaratibu wake,” alisema Abdalla.

Mfanyabiashara mwingine, Rashidi Omary alisema:“Tunalipa ushuru wa Sh1,000 kwa siku kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na kipato chetu.”

Wakati wafanyabiashara wakitoa maoni hayo, kazi inayoonekana kuwa nzito ni kuwatambua wanaostahili.

“Kufungua bucha, saluni au mgahawa kuna utaratibu wake. Hawa hawatahusika na wataendelea kulipa ushuru wa soko kwani ni lazima lijiendeshe,” alisema Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara jana.

“Hivi ni vitambulisho vya wamachinga ambao walikuwa hawatambuliki kisheria.”

Machinga, jina ambalo awali lililotokana na wafanyabiashara kutoka kabila la Wamachinga, huzunguka na bidhaa mitaani na hivyo huonekana zaidi mijini kuliko kwenye makazi wanayoishi, hali inayoweza kufanya kazi ya kuwatambua kuwa ngumu.

Lakini mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri aliiambia Power Breakfast ya kituo cha Clouds FM kuwa ataitisha mikutano ya taasisi za Serikali za eneo husika, watendaji na wanajamii ili kuwatambua wafanyabiashara hao na kuwapa vitambulisho.

Katika kile kinachoonyesha kuepuka kadhia hiyo, mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ameamua kuwashushia jukumu hilo wakuu wa wilaya zake tano na kuwapa vitambulisho hiyo.

Mtaka pia aliitisha kikao cha wakuu hao wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri sita, watendaji na viongozi wa vijiji kwa ajili ya kujadili suala hilo jana.

Alisema ili kufanikisha mpango huo watakwenda katika kila mikusanyiko ya biashara kama magulio kwa ajili ya kutoa elimu.

Hata hivyo, rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), Fatma Karume alikuwa na maoni tofauti.

“Lazima (kwanza) sheria ya vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ipitishwe, itoe description (ufafanuzi) ya nani ni mfanyabiashara mdogo na kiwango gani anatakiwa kulipa na anapata wapi hivyo vitambulisho,” alisema.

Alisema kuwepo kwa sheria kutasaidia kuwa na utekelezaji unaolingana kwa mikoa yote, kufuatilia pamoja na kuwapa fursa wafanyabiashara kudai haki zao pale zinapokiukwa.

Imeandikwa na Cledo Michael na Jackline Masinde (Dar), Florah Temba (Moshi), Nazael Mkiramweni (Dodoma), Burhani Yakub (Tanga), Ipyana Samson (Mbeya) na Hamida Shariff (Morogoro).

Soko Kuu la Mwanjelwa, Dickson Kalapila alisema Serikali iandae utaratibu maalumu wa kuwatambua katika maeneo yao kabla ya kugawa vitambulisho hivyo ili wasipewe wasiostahili.

“Tunashukuru Rais anatupigania, lakini watendaji wake wa chini wanashindwa kumuelewa, matokeo yake kila siku wanakuwa na migogoro na wamachinga kwa kuwatengea maeneo ambayo si rafiki kwa biashara zao,” alisema Dickson.

Muuza mboga wa Soko la Sido, Halima Anania alisema: “Wafanyabiashara wengi wadogo tunaendesha biashara zetu kwa mikopo, hivyo kupitia vitambulisho hivyo vitatuwezesha kufanya biashara kwa uhuru.”

Tanga

Muuza viatu vya mitumba katika gulio la Tangamano mkoani Tanga, Titus Masawe alisema taasisi za fedha nazo kama zitaweka utaratibu wa kuwatambua na kuwakopesha mitaji, itawainua kiuchumi.

“Wasiishie kutupatia vitambulisho pekee, tuwekewe utaratibu wa kutambulika kwenye vyombo vya fedha tuweze kukopeshwa na kukuza mtaji,” alisema Masawe.

Dodoma

Mmoja wa wamachinga waliozungumza na Mwananchi jijini hapa, Nasibu Jaha alisema vitambulisho vya Rais Magufuli vitasaidia kuziba mianya ya rushwa iliyokuwa inasababisha kupoteza bidhaa zao kila wanapokamatwa.

“Unakuta mtu kakamatwa akifika ofisi za jiji, lazima atoe chochote ili aondoke na mzigo wake akikosa anaucha, sasa ataenda kuuza nini?” alihoji Jaha.

Alisema sasa vitasaidia kuwaepusha na kero sugu ya kukamatwa hovyo na askari mgambo. Mfanyabiashara mwingine, Sarah Yusto alisema mtaji wake ni Sh1 milioni, lakini TRA walimuweka kwenye kundi la mtaji wa Sh20 milioni.

“Tunashukuru Rais kuwatambua wajasiriamali wadogo, tulichokuwa tunafanyiwa ni sawa na mtoto wa darasa la kwanza umpeleke kidato cha kwanza,” alisema Yusto.

Kilimanjaro

Mfanyaabiashara wa urembo katika Stendi Kuu ya Mabasi mjini Moshi, Alhaj Abdala alisema watahitaji ufafanuzi kutoka kwa uongozi wa stendi hiyo na ule wa wamachinga kwa kuwa wanaweza kupewa vitambulisho lakini baadaye wakatakiwa kulipa ushuru.

ishwa na biashara tunayofanya. Tukipewa vitambulisho na kulipa Sh20,000 kwa mwaka ni neema kwetu. Tumeambiwa kitatuwezesha kufanya biashara mahali popote, hili ni jambo zuri,” alisema Omary.Tamisemi

Ingawa TRA ndiye yenye mamlaka ya kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria, Rais Magufuli aliipa Wizara ya Ofisi ya Rais; Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) jukumu la kugawa viutambulisho kwa wamachinga ambao wanaingizwa kwenye mfumo wa kulipa kodi.

Naibu waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara alisema tayari wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo ya namna ya kuwaainisha na kuwafikia walengwa.

“Hivi ni vitambulisho vya wamachinga ambao walikuwa hawatambuliki kisheria,” alisema Waitara.

Alifafanua kuwa vitambulisho hivyo havitawahusu wafanyabiashara waliopo kwenye masoko wanaofanya biashara rasmi kwani kila moja inautaratibu wake.

“Kufungua bucha, saluni au mgahawa kuna utaratibu wake. Hawa hawatahusika na wataendele akulipa ushuru wa soko kwani ni lazima lijiendeshe…wanahitaji maji, ulinzi hata usafi. Haya yote yanahitaji kugharamiwa,” alifafanua kuhusu uchangiaji wa gharama nyingine.

Licha ya vitambulisho hivyo, Rais aliitaka TRA kurekebisha kodi ya majengo ili wananchi wengi zaidi wajisajili na kuilipa kwa hiyari yao wenyewe.

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume amesema maagizo ya Rais yanakiuka misingi ya sheria.

Alisema kuitaka TRA kushusha kodi ya majengo kutaathiri utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19 iliyoitisha vyanzo vya mapato ikiwamo kodi hiyo.

Fatma alisema maagizo yote mawili yapo kinyume na sheria ingawa yanaweza kuwa na faida kwa wananchi.

“Lazima sheria ya vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ipitishwe itoe description (ufafanuzi) ya nani ni mfanyabiashara mdogo na kiwango gani anatakliwa kulipa na unapata wapi hivyo vitambulisho,” alisema

Alisema uwepo wa sheria utasaidia kuwa na utekelezaji unaolingana kwa mikoa yote, kufanya ufuatiliaji pamoja na kuwapa fursa wafanyabiashara wadogo kudai haki zao pale zinapokiukwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya kodi, nyumba ya kawaida ni Sh10, 000 (flat rate) nyumba ya ghorofa ni Sh50, 000 kwa sakafu (floor).

Imeandaliwa na Cledo Michael, Jackline Masinde, Florah Temba, Nazael Mkiramweni, Burhani Yakub, Ipyana Samson, Hamida Shariff,