Waziri wa zamani aieleza mahakama chanzo cha kujiuzulu

Muktasari:

Ni Paul Kimiti, Waziri wa zamani wa Kilimo ambaye leo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chanzo cha kujiuzulu ujumbe wa bodi  ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)


Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo wa zamani, Paul Kimiti(73) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alijiuzulu ujumbe wa bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) baada ya kubaini menejimenti ya shirika hilo kukodisha ndege ya aina ya Airbus 320 bila kufuata utaratibu.

Kimiti ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 12, 2018 mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa ATCL, David Mattaka.

Kesi hiyo ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh71bilioni inamkabili Mattaka na wenzake wawili.

"Nilijiuzulu ujumbe wa bodi ya ATCL mwaka 2009 baada ya menejimenti ya ATCL kufanya uamuzi wa kukodisha ndege aina Airbus 320 bila kushirikisha bodi,” amedai Kimiti ambaye ni shahidi wa 16 katika kesi hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi