Kiwanda cha Mtibwa, Jeshi la Polisi wadaiwa mamilioni na Tanesco

Muktasari:

Meneja wa Tanesco, Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy amesema taasisi hizo kwa ujumla zinadaiwa na Tanesco kaisi cha Sh6bilioni.

Morogoro.Shirika la ugavi wa umeme (Tanesco) Mkoani Morogoro limeendelea kuzikatia umeme taasisi mbalimbali za Serikali na zile za binafsi kikiwamo kiwanda cha sukari cha Mtibwa na Jeshi la Polisi.

Meneja wa Tanesco, Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy amesema taasisi hizo kwa ujumla zinadaiwa na Tanesco kaisi cha Sh6bilioni.

Tanesco kimesema kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kinadaiwa Sh2bilioni na jeshi la polisi linadaiwa zaidi ya Sh300milioni.