Kiwira kuiingizia Serikali hasara ya mabilioni ya fedha

Muktasari:

Eneo la mgodi huo lililopo hatarini kulipuka ni la Mlima wa Ivogo ambalo shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa kwenye handaki ambalo kitaalamu huhitaji kupozwa wakati wote.

Mbeya. Mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira uliopo mkoani Mbeya upo hatarini kulipuka siku chache zijazo na kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya fedha iwapo hatua za haraka za kurejesha umeme hazitachukuliwa.

Eneo la mgodi huo lililopo hatarini kulipuka ni la Mlima wa Ivogo ambalo shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa kwenye handaki ambalo kitaalamu huhitaji kupozwa wakati wote.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa pamoja na mgodi huo kutakiwa kupozwa wakati wote, una zaidi ya miezi mitatu haujapozwa baada ya Tanesco kukata umeme tangu Februari, kutokana na deni la Sh1.3 bilioni.

 

Kaimu meneja mkuu wa mgodi huo, Moses Mapamba alimwambia mwandishi wetu aliyetembelea mgodi huo hivi karibuni kuwa kuna hatari mbili zinazoweza kusababisha mlipuko ikiwamo kemikali inayoitwa ‘Methane (CH4)’.

Alipouliza kwa simu, Waziri wa Nishati na Madini (kabla ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo), Profesa Sospeter Muhongo alisema hana taarifa za hatari ya kulipuka kwa mgodi huo, huku akimtaka mwandishi kufuatilia sababu ya Tanesco kukata umeme.

Habari kamili soma Gazeti la Mwananchi