Friday, February 17, 2017

Kizimbani kwa kukutwa na gramu 95.8 za heroine

 

By Jesse Mikofu na Jonathan Musa, Mwananchi

Mwanza. Watu watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mwanza kwa kosa la kukutwa na gramu 95. 8 za dawa za kulevya aina ya heroine.

Akisoma mashtaka leo mbele ya hakimu mkazi, Veronica Mugendi, Wakili wa Serikali, Lilian Meli alidai kuwa mshatakiwa Khasim Mohamed (43), anashatakiwa kwa kosa moja la kukutwa na dawa za kulevya kinyume cha sheria.

Meli alidai kuwa mshatakiwa huyo kesi namba 46/2017, dawa hizo katika maeneo ya Kanyerere Kata ya Mahina jjini Mwanza.

Hata hivyo mshatakiwa alikana shtaka hilo na kuomba kupewa dhamana dhidi ya kesi inayomkabili

Mshtakiwa alishindwa kukidhi vigezo vya masharti ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao walitakiwa kusaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja na wawe na barua za utambulisho kutoka kwa mwenyekiti wa Serikali za mtaa.

Baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana hiyo alirudishwa rumande mpaka Machi 2 mwaka huu ambapo kesi hiyo itakapotajwa tena.

-->