Kizungumkuti chaibuka ununuzi wa pamba

Muktasari:

Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima wa Pamba nchini, George Mpanduji ameiomba Serikali kuutafutia ufumbuzi wa haraka mgogoro wa ununuzi wa zao hilo.

Kahama. Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima wa Pamba nchini, George Mpanduji ameiomba Serikali kuutafutia ufumbuzi wa haraka mgogoro wa ununuzi wa zao hilo.

Mpanduji amesema hayo kufuatia wanunuzi wa zao hilo kugoma wakishinikiza Serikali kuondoa ongezeko la Sh200 kwa kilo katika bei elekezi ya Sh1, 000 iliyotangazwa hivi karibuni. 

Aliitaka Serikali kudanya hivyo ili kuwaondolea kero wakulima ambao wamebaki njia panda wasijue pa kuuzia zao hilo baada ya mavuno. 

“Serikali ipunguze utitiri wa kodi na ushuru wa mazao kuanzia zile zinazotozwa na Serikali kuu na halmashauri za wilaya. Hii itapunguza gharama za uendeshaji kwa makampuni na wanunuzi wa pamba,” alishauri Mpanduji