Kocha Unai Emery atangazwa rasmi kumrithi Wenger

Muktasari:

Mfaransa Wenger amedumu kwenye nafasi hiyo kwa takribani miaka 22 akiifundisha klabu hiyo inayotumia dimba la Emirates.

England. Uongozi wa Arsenal umemtangaza rasmi leo Jumatano, Unai Emery kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akimrithi Arsene Wenger.
Mfaransa Wenger amedumu kwenye nafasi hiyo kwa takribani miaka 22 akiifundisha klabu hiyo inayotumia dimba la Emirates.
Emery ambaye aliwahi kuifundisha PSG anachukua rasmi mikoba hiyo kukinoa kikosi cha Arsenal huku akiwa ameitumikia PSG kwa takribani miaka miwili.
Tetesi za kocha huyo kutua Arsenal, zilianza kuvuja tangu jana usiku na sasa uongozi wa klabu hiyo umethibitisha rasmi.
Mtandao wa Arsenal uliweka taarifa leo Jumatano ikisomeka kuwa, “Unai Emery ndiye amekuwa kocha wetu mpya”.