Kongamano la kuchochea uwekezaji nchini kufanyika India Agosti 30

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe

Muktasari:

  • Akizungumza leo Jumanne, Agosti 15 na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe amesema lengo la mkutano huo ni kutangaza fulsa za biashara na uwekezaji zilizopo hapa nchini.

Dar ea Salaam. Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo Nje pamoja na wafanyabiashara wenye viwanda nchini India wameandaa kongamano maalumu la kuhamasisha na kukuza uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza leo Jumanne, Agosti 15 na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe amesema lengo la mkutano huo ni kutangaza fulsa za biashara na uwekezaji zilizopo hapa nchini.

Mwambe amesema kuwa uwekezaji huo ni katika sekta mbalimbali kama vile viwanda, kilimo na usindikaji wa mazao, afya, teknolojia ya habari na mnawasiliano pamoja na madawa.

Kongamano hilo litakalofanyika Agosti 30 nchini India litahudhuriwa na wawekezaji wa kampuni kubwa zaidi ya 100 kutoka India ambazo zitasaidia kuitangaza Tanzania.

Mwambe amekaribisha kampuni za Kitanzania na sekta binafsi kushiriki kwenye kongamano hilo ili kuweza kuanzisha, kukuza na kuendeleza ushirikikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji kwa kushirikiana na kampuni za India.