Korti yatupa kesi dhidi ya Pierre Nkurunziza

Rais wa Burundi,Pierre Nkurunzinza

Muktasari:

Taasisi hizo zilikuwa zinadai kuwa katiba ya Burundi inazuia mtu kuongoza nchi kwa vipindi vitatu.

Arusha. Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na taasisi tatu za kiraia kupinga uhalali wa Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.

Taasisi hizo zilikuwa zinadai kuwa katiba ya Burundi inazuia mtu kuongoza nchi kwa vipindi vitatu.

Jaji wa mahakama hiyo, Isack Lenaola amesema walalamikaji katika kesi hiyo,  Jukwaa la Asasi za Vyama vya Kiraia vya Nchi za Afrika Mashariki (EACSOF), Chama cha Wanasheria wa Afrika (Palu) na Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) walifungua kesi hiyo nje ya muda.

Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Katibu Mkuu wa EAC, Tume ya Uchaguzi ya Burundi (Ceni) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Burundi.

Hata hivyo, Jaji alisema Ceni iliondolewa kutokana na kutokuwa na sifa ya kushtakiwa katika mahakama hiyo.