VIDEO-Kubenea: Waliobomolewa Kimara, Ubungo wafidiwe

Muktasari:

Amesema ubomoaji huo umefanyika wakati Mahakama ilitoa amri ya nyumba hizo kutobomolewa.

 


Dodoma. Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameitaka Serikali kuwalipa fidia wakazi wa Ubungo na Kimara jijini Dar es Salaam kwa kuwavunjia nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro.

Amesema ubomoaji huo umefanyika wakati Mahakama ilitoa amri ya nyumba hizo kutobomolewa.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo Aprili 23, 2018, Kubenea amesema, “Nasikitika Serikali kuvunja nyumba za wakazi wa Ubungo, Kimara na maeneo mengine licha ya mahakama kuzuia ubomoaji.”

“Ubomoaji umefanyika kinyume na taratibu kwa kuwa Benki ya Dunia (WB) imesitisha kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo, nataka Serikali iwafidie wananchi wa Ubungo kutokana na nyumba zao kuvunjwa.”

Amesisitiza,“Kwa sasa Serikali italazimika kulipa fidia ili mradi uendelee sasa watalipaje wakati nyumba zimevunjwa.  Inakuwaje mnabomoa nyumba zilizopo umbali wa mita 200 kutoka barabara kubwa?”