Kuna wanafunzi 1400 wenye usonji nchini

Muktasari:

Naibu Waziri ameagiza Wakurugenzi kuhamisha walimu wote waliosomea elimu maalumu na kuwapeleka katika shule zenye uhitaji.


Dodoma. Hadi sasa Tanzania ina jumla wanafunzi 1,416 wenye usonji na walimu 157 walio katika shule 18 za msingi.

Kauli hiyo hiyo imetolewa bungeni  leo Aprili 18 na Naibu Waziri ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda ambaye amesema kuwa idadi ya walimu hao haitoshi.

Alikuwa akijibu swali la msingi la Salma Kikwete (mbunge wa kuteuliwa) ambaye alitaka kujua Serikali inawasaidiaje watoto wenye usonji ili nao wapate elimu na kama walimu waliopo wanatosha kwa wahitaji hao.

Katika swali la nyongeza Salma  amesema kwa idadi ya wanafunzi hao walihitaji walimu 283 kwa maana ya watoto watano kwa mwalimu mmoja hivyo kuna upungufu wa walimu 126 akiomba kuajiriwa

Naibu Waziri ameagiza wakurugenzi kuhamisha walimu wote waliosomea elimu maalumu na kuwapeleka katika shule zenye uhitaji pamoja na kuajiri walimu waliosomea elimu hiyo walioko mitaani kwa sasa