Kundambanda kuzikwa leo

Aliyekuwa Mchekeshaji maarufu kutoka kundi la Vituko Show, Ismail Makombe maarufu Baba Kundambanda wakati wa uhai wake

Muktasari:

Pia, Kundambanda aliyekuwa mwanasiasa aligombea ubunge wa Jimbo la Masasi mkoani Mtwara kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu  2015.

Dar es Salaam.  Mchekeshaji maarufu kutoka kundi la Vituko Show, Ismail Makombe maarufu Baba Kundambanda, aliyefariki dunia jana atazikwa leo saa kumi jioni nyumbani kwao Masasi mkoani Mtwara.

Pia, Kundambanda aliyekuwa mwanasiasa aligombea ubunge wa Jimbo la Masasi mkoani Mtwara kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu  2015.

Naibu Katibu mkuu wa CUF Tanzania Bara, Shaweji Mketo alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba, Kundambanda ameacha pengo kubwa kwao.

Wakati wa uhai wake, Kundambanda pia, alikuwa mtunzi wa nyimbo za kuhamasisha harakati mbalimbali za jamii.