Kuzungumza Kiswahili ni kudumisha utamaduni- Salma Kikwete

Mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Salma Kikwete amesema siyo kila mtu anayezungumza Kiswahili katika sehemu mbalimbali hajaenda shule, bali anadumisha utamaduni wa Kitanzania.

Muktasari:

  • Mama Salma ambaye ni Balozi wa Kiswahili barani Afrika ametoa kauli hiyo katika hafla ya utoaji tuzo za waandishi wa fasihi na utunzi jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Salma Kikwete amesema siyo kila mtu anayezungumza Kiswahili katika sehemu mbalimbali hajaenda shule, bali anadumisha utamaduni wa Kitanzania.

Mama Salma ambaye ni Balozi wa Kiswahili barani Afrika ametoa kauli hiyo katika hafla ya utoaji tuzo za waandishi wa fasihi na utunzi jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Kampuni ya Alaf inayojihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali yakiwamo mabati.

Mama Salma amesema mtu akizungumza Kiswahili huonekana mshamba ambaye hajaenda shule na kiwango chake cha elimu kinaonekana hata darasa la pili hajafika.