Lishe duni yaathiri watoto

Muktasari:

Amesema kutozingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora kunasababisha ongezeko la watoto wenye upungufu wa damu.

Shinyanga. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Ntuli Kaporogwe amesema asilimia 71 ya watoto mkoani hapa wanakabiliwa na matatizo ya upungufu wa damu mwilini.

 Amesema kutozingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora kunasababisha ongezeko la watoto wenye upungufu wa damu.

Dk Kaporogwe amesema licha ya mkoa huo kuwa na chakula cha kutosha, wazazi wanashindwa kuzingatia matumizi ya lishe bora hivyo kuibua matatizo ya afya kwa watoto kukosa damu.

“Asilimia 70 ya chumvi inayouzwa mkoani Shinyanga haina madini joto na  kuleta madhara kwenye ubongo wa binadamu kuanzia akiwa mtoto mdogo,” alisema.