Lissu aitwa kortini leo

Muktasari:

Hakimu Thomas Simba ametoa agizo hilo jana baada ya Lissu pamoja na mdhamini wake kutokuwapo mahakamani hapo kama sheria inavyotaka.

Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio, ametakiwa kufika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujieleza kwa nini asifutiwe dhamana.

Hakimu Thomas Simba ametoa agizo hilo jana baada ya Lissu pamoja na mdhamini wake kutokuwapo mahakamani hapo kama sheria inavyotaka.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi kuomba itolewe hati ya kumkamata mbunge huyo, lakini Hakimu Simba akataka leo aje kujieleza kwanini asifutiwe dhamana.