Lowassa ahofia Serikali kuhusu Chadema

Edward Lowassa

Muktasari:

Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani, amesema hayo baada ya kuulizwa kuhusu hali inayoendelea mkoani Arusha kati ya viongozi wa Serikali na Chadema ambayo inaongoza Halmashauri ya Jiji.

Dar es Salaam. Aliyekuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM kabla ya kuhamia Chadema Julai mwaka jana, Edward Lowassa amesema mgogoro unaozidi kukua baina ya viongozi wa mkoa na Chadema ni mpango wa Serikali kutaka kukatisha tamaa vyama vya upinzani ili visitekeleze majukumu yake kwa wananchi.

Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani, amesema hayo baada ya kuulizwa kuhusu hali inayoendelea mkoani Arusha kati ya viongozi wa Serikali na Chadema ambayo inaongoza Halmashauri ya Jiji.

 “Serikali inataka kukatisha tamaa vyama vya upinzani ili visitekeleze majukumu yake,” amesema Lowassa akiwa nyumbani kwake Monduli mkoani Arusha.

“Kinachoendelea mkoani Arusha ni mkakati wa Serikali kukandamiza upinzani na kuwakatisha tamaa ili wasifanikiwe katika majukumu yao.”