Lukuvi afuta hati tano za umiliki wa ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuki amesema hati hizo zilizofutwa zilitolewa kwa udanganyifu kwa mmiliki huyo katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Simiyu.

Dar es Salaam. Serikali imefuta hati 5 za umiliki wa ardhi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na raia wa Uingereza aliyetajwa kwa jina la Hamant Patel mkazi wa Mwanza baada ya kugundulika kughushi cheti cha kuzaliwa na kujitambulisha kama raia wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuki amesema hati hizo zilizofutwa zilitolewa kwa udanganyifu kwa mmiliki huyo katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Simiyu.

Habari zinazohusiana

Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa sheria za nchi raia wa nje hawaruhusiwi kumiliki ardhi na kwamba wanayo fursa ya kupata ardhi kupitia kituo cha uwekezaji nchini (TIC).