Lukuvi atua Tabora kutatua migogoro ya ardhi

Waziri wa Ardhi,William Lukuvi,akisalimiana na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tabora,Seleman Kameya huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa,Emmanuel Nley,akiangalia.

Muktasari:

Katika ziara hiyo, waziri huyo atakwenda eneo la Malabi manispaa ya Tabora na kuzungumza na viongozi mbalimbali

Tabora. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi leo Alhamisi Septemba 20, 2018 ameanza ziara ya kikazi mkoani hapa kushughulikia migogoro ya ardhi.

Katika ziara hiyo, waziri huyo atakwenda eneo la Malabi manispaa ya Tabora na kuzungumza na viongozi mbalimbali.

Pia atatatua migogoro ya muda mrefu ya ardhi, ikiwemo ile ya wananchi na taasisi za Serikali, yakiwemo majeshi.

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa habari zaidi