MCL yachangia Sh10 milioni tetemeko la ardhi Kagera

Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai akizungumzia mchango wao walioutoa kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.

Muktasari:

  • Akizungumza wakati wa kunadi mechi ya leo ya wabunge kuchangia waathirika wa maafa hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai amesema ni kawaida MCL kupitia gazeti la Mwanaspoti kushiriki kila linapojitokeza jambo linalohusu michezo.

Dar es Salaam. Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) imetoa mchango wa Sh10 milioni kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

Akizungumza wakati wa kunadi mechi ya leo ya wabunge kuchangia waathirika wa maafa hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai amesema ni kawaida MCL kupitia gazeti la Mwanaspoti kushiriki kila linapojitokeza jambo linalohusu michezo.

 “Mbali ya fedha hizo, tumekuwa tukitoa mchango wetu kama wanahabari wa kueleza kwa kina kinachoendelea huko, jambo ambalo linaisaidia Serikali na jamii nzima kufahamu ukubwa wa tatizo na nini kinapaswa kufanyika,”amesema.