MV Umoja kurudisha hadhi ya usafiri Kanda ya Ziwa

Muktasari:

Kauli  hiyo imetolewa na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua Bandari hiyo kuangalia maendeleo yake leo, na kuitaka Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Shirika la Reli Nchini (TRL), na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL),  kuanza kuandaa Mfumo mmoja wa kutoa Stakabadhi ili kuwarahisishia wateja wake huduma za usafirishaji wa mizigo.

Imeelezwa kuwa kukamilika kwa ukarabati wa meli ya MV Umoja kutarudisha huduma ya usafirishaji wa mizigo katika kanda ya ziwa kupitia bandari ya Kemondo iliyopo mkoani Kagera.

Kauli  hiyo imetolewa na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua Bandari hiyo kuangalia maendeleo yake leo, na kuitaka Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Shirika la Reli Nchini (TRL), na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL),  kuanza kuandaa Mfumo mmoja wa kutoa Stakabadhi ili kuwarahisishia wateja wake huduma za usafirishaji wa mizigo.

Waziri Mbarawa ameitaka TRL kukarabati njia za reli bandarini hapo haraka iwezekanavyo ili kuruhusu mizigo itakayokuja ikiwa kwenye mabehewa kwa njia ya meli iweze kupakuliwa pindi Meli hiyo itaposhusha.