Ma-RC Kaskazini waanza utekelezaji

Muktasari:

  • Imeelezwa kuwa uamuzi huo unatokana na agizo la Rais John Magufuli aliyetaka mafuta yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Tanga yauzwe kwa bei ya chini.

Wakuu wa mikoa ya Kaskazini wamejiwekea mkakati endelevu wa kukagua mafuta kwenye vituo vyote vilivyo katika maeneo yao.

Imeelezwa kuwa uamuzi huo unatokana na agizo la Rais John Magufuli aliyetaka mafuta yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Tanga yauzwe kwa bei ya chini.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela alisema pamoja na wenzake; Joel Bendera wa Manyara, Anna Mghwira wa Kilimanjaro na Mrisho Gambo wa Arusha, wameweka mkakati wa pamoja wa kufanya ukaguzi wa kila kituo ili kujua kama yanauzwa kwa bei inayolingana na yalikotolewa.

Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa maghala ya Kampuni ya GBP Jijini Tanga, Rais Magufuli alisema ameamua kutoa agizo hilo ili uwekezaji uliofanywa na GBP Jijini Tanga, wa maghala ya kupokea mafuta kutoka nchi za Uarabuni yaweze kuuzwa kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini, utakasaidia kuondoa msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam. “Lazima tusimamie bei ya mafuta ili uwekezaji uliofanywa na GBP hapa Tanga uwe na tija,” alisema Rais Magufuli.

na usaidie kuondoa msongamano wa maroli ya

mafuta Jijini Dar es salaam”alisema Rais Magufuli.

Waziri wa Viwanda,biashara na masoko,Charles Mwijage alisema maghala ya

GBP Tanga ni ya pili kwa ukubwa na uwezo wa kuhifadhi lita 122.6

milioni za mafuta huku ikilipa Serikalini kiasi cha sh 293.263 bilioni

za kodi ambapo TIPA ya jijini Dar es salaamni ya kwanza.

Waziri Mwijage alisema GBP Tanga itakuwa ni ghala la akiba ya Taifa ya

mafuta likiwa tayari kuhudumia iwapo Dar es salaam kutakuwa na uhaba

au tatizo la upatikanaji wa bidhaa hiyo.