Maalim Seif ampuuza Jecha

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

Muktasari:

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha kituo cha televisheni cha Azam TV juzi, Jecha alisema hakumshirikisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 visiwani humo.

Dar es Salaam.  Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema ameshamalizana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha na haoni umuhimu wa kuzungumzia wala kumjibu, kwa sababu atampa sifa asizostahili.

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha kituo cha televisheni cha Azam TV juzi, Jecha alisema hakumshirikisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 visiwani humo.

Jecha alifuta matokeo hayo Oktoba 28, 2015, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa uchaguzi wa rais, huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.

Alitangaza uchaguzi mpya Machi 20, 2016 ambao ulisusiwa na CUF na Dk Shein kuibuka mshindi.