Maambukizo ya malaria yaongezeka

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema maambukizo ya ugonjwa wa malaria yameongezeka kwa asilimia 100.

Muktasari:

Mwalimu ametoa takwimu hzi jana alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya afya uliokuwa ukijadili Sera ya Afya.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema maambukizo ya ugonjwa wa malaria yameongezeka kwa asilimia 100, baada ya kupanda kutoka asilimia saba mwaka 2010 mpaka kufikia 14 kwa mwaka huu.

Mwalimu ametoa takwimu hzi jana alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya afya uliokuwa ukijadili Sera ya Afya.

 “Kuongeza kwa malaria ni tatizo katika nchi yetu na takwimu za mwaka 2016 zimeonyesha kwamba yameongezeka kutoka asilimia saba mwaka 2010 mpaka asilimia 14 kwa hiyo tumerudi kwa mara mbili ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita,” amesema Mwalimu.