Madaktari wanaomiliki maduka ya dawa kuchunguzwa

Muktasari:

  • Amesema ameshangazwa kukuta maduka ya dawa yanayomilikiwa na madaktari nje ya hospitali hiyo kwani tayari Serikali ilishaagiza kuondolewa kwa maduka ya madaktari karibu na hospitali wanazofanyia kazi.

Mafia. Miezi saba baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dk Beatrice Byalugaba kufanya uchunguzi na kubaini madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia wanaomiliki maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo na kuwachukulia hatua.

Amesema ameshangazwa kukuta maduka ya dawa yanayomilikiwa na madaktari nje ya hospitali hiyo kwani tayari Serikali ilishaagiza kuondolewa kwa maduka ya madaktari karibu na hospitali wanazofanyia kazi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Eric Mapunda ameiiomba Serikali iwape kibali cha kununua dawa zinazokosekana Bohari ya Dawa (MSD) moja kwa moja bila ya kupitia utaratibu wa ununuzi wa umma.