Sunday, October 23, 2016

Madiwani Arusha kulipwa posho Sh10,000

 

By Moses Mashalla, Mwananchi mmashalla@mwananchi.co.tz

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro wamesisitiza kuwa posho ya madiwani itakuwa Sh10,000 kwa kikao kitakachomalizika na endapo kitavunjika hawatalipwa.

Viongozi hao walitoa msimamo huo kwa nyakati tofauti wakati wakifunga Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa.

Gambo amesema msimamo wa posho za vikao kwa madiwani uko palepale na kuongeza kwamba endapo watavunja kikao chochote cha baraza la madiwani hakuna kulipwa.

Daqaro ameunga mkono hoja hiyo akisema msimamo wa posho ni uleule wa Sh10,000 na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kusimamia suala hilo.

-->