Maghembe azuia vibali kwa wavunaji magogo wasio na mipango

. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe

Muktasari:

  • Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kuangalia utekelezaji wa mapendekezo ya utafiti wa Shirika la Kimataifa la Traffic 'Traffic report review' ya  2007.

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amepiga marufuku utoaji vibali kwa wavunaji wa misitu wasiokuwa na mipango ya uendelezaji wa misitu. 

 

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kuangalia utekelezaji wa mapendekezo ya utafiti wa Shirika la Kimataifa la Traffic 'Traffic report review' ya  2007.

"Kuanzia sasa kuvuna magogo iwe kwa watu wanaopanda. Siyo kuvuna vuna tu. Inabidi tuanzishe sheria ili kuwa na vyama vya upandaji. Haiwezekani kuendelea na uvunaji holela tu bila kufikiria uhifadhi," amesema Profesa Maghembe.

Mwaka 2007, Shirika hilo lilifanya utafiti uitwao 'Misitu, Utawala bora na Maendeleo ya Taifa'  na kutoa mapendekezo 60 kwa lengo la  udhibiti na uendelezaji wa Misitu nchini. 

 Baada ya mapendekezo hayo 60,  Julai Mwaka jana, Traffic  walifanya utafiti mwingine ili kujiridhisha na utekelezaji wa mapendekezo matano yaliyoelekezwa kwa serikali.