Wednesday, January 11, 2017

Magufuli afyeka Sh36 bilioni ujenzi hospitali ya mkoa SimiyuRais John Magufuli 

Rais John Magufuli  

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Bariadi. Rais John Magufuli amepunguza Sh36bn za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu akidai gharama za ujenzi zimekuwa kubwa mno badala yake ameagiza hospitali hiyo ijengwe kwa gharama ya Sh10 bilioni.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Somanda mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Amesema kuwa kiwango cha Sh46 bilioni zilizopangwa kutumika katika kujenga hospitali hiyo ni kikubwa sana hivyo amesema kuwa Serikali itatoa Sh10 bilioni tu ambazo amedai zitakamilisha ujenzi huo ndani ya mwaka mmoja.

-->