Magufuli amteua Profesa Museru Mkurugenzi wa MNH

Profesa Lawrence Mujungu Museru ameteuliwa kuwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Muktasari:

  • Kabla ya Uteuzi huo Prof Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  amemteua Profesa Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kabla ya Uteuzi huo Prof Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam inaeleza kuwa uteuzi wa Profesa  Museru umeanza jana  Oktoba 2.