Magufuli amtimua Wanyancha Bodi ya Barabara

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Dk James Wanyancha. Picha ya Maktaba

Muktasari:

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Dk James Wanyancha.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo.

Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua Joseph Odo Haule kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo kuanzia leo. Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara.

Wajumbe wengine wa bodi hiyo wanaendelea katika nafasi zao.