Magufuli atengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Kahama

Muktasari:

  • Amteua Anamringi Macha kuwa mkuu wa wilaya hiyo

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo Jumapili Julai 15, 2018 ametengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema kufuatia hatua hiyo, kiongozi mkuu huyo wa nchi amemteua Anamringi Macha kuwa mkuu wa wilaya hiyo.

Inaeleza kuwa Macha anatakiwa kuripoti katika kituo chake cha kazi mara moja.