Mahakama ya mafisadi hii hapa, Jaji Mkuu atembelea kujionea

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimsikiliza Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadi Kitunzi akimuelezea jambo alipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali.

Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mohamed Chande Othman leo ametembelea jingo litakalotumika kuanzisha kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu kama ‘Mahakama ya Mafisadi’.

Jaji Mkuu aliambatana na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali ambao walipewa maelezo mbalimbali kuhusu jingo hilo na Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadi Kitunzi.

Jengo hilo liko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam.