Maharusi waliofariki kwa mafuriko kuzikwa kesho

Arusha. Maharusi Munisi Roy (25) na Nembrice Munyaga (20) waliofariki kutokana na mafuriko Februari 24, wanatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Ilkisongo  Kata ya Sambasha wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Maharusi hao,  walifariki juzi baada ya kuzolewa na mafuriko wakiwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Premio, pamoja na ndugu wengine watatu.

Diwani wa kata ya Sambasha, Roy Sabaya amesema marehemu hao  watazikwa baada ya kukamilika taratibu za mazishi.