Majaji waanza kusoma hukumu kesi ya Babu Seya

Muktasari:

 Babu Seya na Papii Kocha walitoka gerezani baada ya Rais John Magufuli kutangaza msamaha kwa wafungwa 8,157

Dar es Salaam. Majaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu, wameanza kusoma hukumu ya kesi ya Nguza Viking maarufu ‘Babu Seya’ na wanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha.

Rais wa mahakama hiyo, Jaji Slyvian Ore amesema hukumu hiyo itasomwa leo Machi 23, baada ya kukamilisha mahitaji yote na kupitia taarifa za wakata rufaa.

Babu Seya na mwanaye Papii Kocha ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika.

Wanamuziki hao walikuhumiwa kifungo cha maisha zaidi ya miaka 10 iliyopita baada ya kupatikana na makosa ya kuwanajisi watoto.

Rais John Magufuli alitangaza kuwasemehe wafungwa 8,157 wakiwamo wanamuziki hao wakati akihutubia maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.