Majaliwa, Mabeyo watua Kisiwa cha Ukara, waliofariki wafikia 131

Muktasari:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na CDF Mabeyo wamewasili katika kisiwa kilichozama Kivuko cha MV Nyerere

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, (CDF), Venance Mabeyo wamewasili katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe jijini Mwanza.

Majaliwa na Mabeyo wametua Ukara saa 12.21 jioni ya leo Septemba 21,2018 kuungana na waombolezaji kufuatia ajali ya Kivuko cha MV Nyerere wakitumia usafiri wa helikopta.

Wawili hao, wamepokewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro na viongiozi wengine wa Serikali.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas kupitia ukurasa wake wa kijamii amesema waliofariki wamefikia 131.

Taarifa zaidi tutawaletea punde