Majaliwa: Watumishi wa umma fanyeni kazi popote

Muktasari:

  • Amesema ni wajibu wa watumishi wa umma kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania, hivyo atakayeshindwa ni vyema akatafute shughuli nyingine nje ya ajira za Serikali.

Mafia. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma kuwa tayari kufanya kazi popote watakakopangiwa na Serikali kulingana na mahitaji ya eneo husika.

Amesema ni wajibu wa watumishi wa umma kuwatumikia na kuwahudumia Watanzania, hivyo atakayeshindwa ni vyema akatafute shughuli nyingine nje ya ajira za Serikali.

Majaliwa amesema hayo kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mkunguni, wilayani Mafia.

 “Hii ni awamu ya kazi zaidi. Hata kaulimbiu ya Rais ya Hapa Kazi Tu! siyo neno la kufurahisha bali lina malengo yanayowataka Watanzania wote wafanye kazi,” amesema.