Majaliwa ahamia rasmi Dodoma

Kikundi cha ngoma cha JKT kikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati wa mapokezi ya  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amehamia rasmi Dodoma leo  Ijumaa Septemba 30, 2016.

Muktasari:

Majaliwa ametua katika uwanja wa ndege wa Dodoma saa 10.07 jioni akiwa ameongozana na mkewe na kupokewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Walemavu, Jenester Mhagama.

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehamia rasmi mkoani Dodoma Ijumaa Septemba 2016.

Majaliwa ametua katika uwanja wa ndege wa Dodoma saa 10.07 jioni akiwa ameongozana na mkewe na kupokewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Walemavu, Jenester Mhagama.

Baada ya kuwasili alikwenda moja kwa moja kwenye makazi yake mpya yalioko Mlimwa ambako alipokewa na wazee wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wa dini.

Katika Barabara inayoelekea kwenye makazi yake, wakazi wa Dodoma wamesimama kandokando wakimshangilia wakimpungia majani ya miti kama ishara ya amani huku katika lango la kuingilia nyumbani kwake, kukiwa kumejaa Bajaji na pikipiki.