Majaliwa aitaka TCU kuhakiki program za masomo vyuoni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Muktasari:

Majiwali ametoa  agizo hilo leo (Jumanne) wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kuhakikisha programu za masomo zinazoanzishwa na vyuo vikuu nchini zinazingatia mahitaji ya Taifa na soko la ajira.

Majiwali ametoa  agizo hilo leo (Jumanne) wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema hivi sasa kuna baadhi ya vyuo nchini ambavyo vinatoa programu ambazo haziendani na mahitaji halisi ya Taifa pamoja na soko la ajira.

"Napenda kusisitiza TCU inahakikisha programu hizo zinazingatia mahitaji yetu hapa nchini,"amesema.

Habari Zinazohusiana