Majaliwa atoa wiki walimu wahamishwe Kibaha kwenda Rufiji

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 

Muktasari:

Ametoa agizo hilo  jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji.

Ametoa agizo hilo  jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita.

"Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu wamerundikana ,sasa fanya ‘realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji."alisema Waziri Mkuu.

Kwa taarifa hii zaidi na nyingine nyingi  nunua gazeti lako la Mwananchi kesho au soma mtandaoni BONYEZA HAPA