Majambazi wenye silaha wapora mali baa

Muktasari:

Manyama alisema baada ya kuvamiwa, majambazi hao walifyatua risasi hewani na baadaye kupora simu tatu na fedha taslimu Sh90,000.

Musoma. Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia kwa mfanyabiashara Chrismas Manyama (55), mkazi wa Bweri mjini Musoma mkoani Mara, wakiwa na silaha za jadi na bunduki.

Manyama alisema baada ya kuvamiwa, majambazi hao walifyatua risasi hewani na baadaye kupora simu tatu na fedha taslimu Sh90,000.

Alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20, saa moja jioni akiwa eneo lake la biashara za baa na duka lililopo  Mtaa wa Nyabisare.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema watu hao walipora simu za wateja ambazo thamani yake bado haijajulikana na fedha za mauzo ya baa.