Majambazi yauawa, polisi waanza kutoka eneo la tukio

Muktasari:

Milio ya risasi na mabomu vilisikika kuanzia saa saba usiku katika eneo hilo ambalo majambazi hayo walikuwa wamejificha.

Dar es Salaam.Majambazi ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuwawa katika mapigano hayo  kati yao na polisi huko Vikindu, wilaya ya Mkuranga leo.

Milio ya risasi na mabomu vilisikika kuanzia saa saba usiku katika eneo hilo ambalo majambazi hayo walikuwa wamejificha.

Habari zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa  mpaka sasana magari ya polisi yanaonekana yakiingia na kutoka katika eneo la tukio Vikindu kwenye nyumba walimojificha.